Serikali Nchini, imekusudia kuendelea kufanya msako mkali ili wahusika wote wa biashara hiyo haramu wachukuliwe hatua kali, na kuongeza kasi ya mapambano ili kukomesha biashara, kilimo na matumizi ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo, imetolewana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kitaifa Katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Amesema, pia mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zitaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya Rushwa, huku akitoa wito kwa Watanzania kupambana na vitendo vya rushwa.

“Tafiti za taasisi za kitaifa na kimataifa zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa. Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa REPOA iliyotolewa Machi 9, 2022 Tanzania inafanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo zaidi ya asilima 77 ya Watanzania waliohojiwa walikiri kuwa rushwa imepungua nchini,” amefafanua Majaliwa.

Aidha, amesema Serikali kupitia mbio hizio za mwenge itaendelea kuwashirikisha wananchi na wadau wengine katika mapambano dhidi ya maambukizi ya mapya ya virusi vya UKIMWI, na kudai kuwa haiwezekani kufikia ndoto tulizojiwekea kimaisha bila kuwa na afya njema, hivyo wananchi washiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Dkt. Jafo ahimiza matumizi nishati safi ya kupikia
Wataalam BMH watoa sarafu kwenye koo la mtoto