Kocha Mkuu wa Sporting CP, Ruben Amorim, amepuuzilia mbali uvumi kuhusu hatma yake na kusema kwamba kushinda mataji msimu huu katika klabu hiyo ya Ureno ndicho kipa umbele chake kikuu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 39, amekuwa akihusishwa na kuchukua jukumu la kuinoa Liverpool, huku Jurgen Klopp akitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Uvumi kuhusu mustakabali wa Amorim umeshika kasi katika siku za hivi karibuni huku bosi wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso akisema mustakabali wake ni kubakia kwenye klabu hiyo ya Bundesliga.

“Kocha wa Sporting ndio pekee wa Sporting.” alisisitiza Amorim.

“Wachezaji ni kiasi gani wanataka kushinda na wanajua kushinda na ninataka kushinda mataji mataji kwa Sporting. Wako wazi k kwamba kila  mtu analenga kushinda mataji”

Amorim alikejeli ripoti kwamba kila mtu analenga kwamba Sporting tayari wamepanga mrithi wake, Anthony Barry mwenye umri wa miaka 37, ambaye ni Kocha Msaidizi wa Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Ureno.

“Kitu pekee kinachoniudhi ni kwamba tayari walikuwa na mbadala wangu,” alitania Amorim.

“Hilo ndilo lililonikera zaidi, hata nilimwambia Viana Hugo Viana, Mkurugenzi wa Soka wa Sporting atulie kwa sababu si hivyo.”

Mtindo wa uchezaji wa kushambulia wa Amorim umevutia watu wengi katika miaka yake minne ya kuinoa Sporting na tayari ameshinda taji la Ligi ya Ureno na mataji mawili ya ligi katika klabu hiyo.

MAKALA: Faye amebeba tumaini jipya la Wasenegali
Simba SC yawasili salama Cairo