Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula, amejiuzulu wadhifa huo pamoja na kiti cha ubunge, ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama kutupilia mbali ombi lake la kuzuia kukamatwa kwa tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Nqakula amesema anataka kutumia muda wake kushughulikia uchunguzi ulioanzishwa dhidi yake, kuhusiana na tuhuma hizo.

Nqakula anatuhumiwa kupokea hongo ya dola 135,000 kutoka kwa mkandarasi mmoja wakati alipokuwa akitumikia nafasi ya Uwaziri wa Ulinzi.

Inaarifiwa kuwa, alipatiwa kitita hicho kati ya Desemba 2016 na Julai 2019 na fedha nyingine ya rushwa ya zaidi ya kiasi dola 100,000 hazikulipwa, madai ambayo Nqakula  anayakanusha na kusema uamuzi wake wa kujiuzulu haumaanishi kwamba anakiri tuhuma zinazomkabili.

Siku ya Afya Duniani: Tuchunguze afya zetu - DC Nguli
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 4, 2024