Serikali ya Uingereza imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kutoa shilingi Bilioni 45, ili kusaidia kufanikisha huduma za uzazi wa mpango nchini.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumpokea Waziri wa Maendeleo na Maswala ya Afrika kutoka Uingereza, Andrew Mitchell, aliyetembelea Zahanati ya Vingunguti na kujionea huduma za uzazi wa mpango zinavyotolewa.

Amesema, ufadhili huo ni matunda mazuri ya juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Uingereza.

“Kupanga uzazi ni sehemu muhimu ya afya ya mama na mtoto, inayosaidia jamii kupata nafasi ya kuzingatia uzazi na kuhakikisha usalama wa mama na mtoto unapatikana kwa kuacha nafasi baina ya mtoto mmoja na mwingine, hasa katika kipindi cha unyonyeshaji, ili kila mtoto apate muda sahihi wa kunyonya pale anapozaliwa,” alisema Dkt. Mollel.

Naye huyo Waziri huyo kutoka Uingereza, amesema kuwa lengo la ufadhili huo ni kuwawezesha Watanzania, hususan vijana kufanya maamuzi sahihi kuhusu wakati wanapotaka kuwa na watoto ili kuhakikisha shughuli za uzazi hazikwamishi shughuli za maendeleo nchini.

“Kupitia ufadhili huu, vijana watapata elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali kama vile UKIMWI na kuelewa umuhimu wa kutumia uzazi wa mpango katika familia zao ili kusaidia taifa kuwa na mpangilio mzuri wa watoto kupishana na kupeana muda wa kunyonya. alisema Mitchell.

SIMULIZI: Ilinibidi, hata kama ni wewe ungefanyaje
Mradi LTIP kuboreshaji usalama wa umiliki ardhi