Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Kagera, Naziri Karamagi amewataka Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji kubainisha changamoto zilizopo kwenye maeneo yao, ili zitatuliwe kabla ya uchaguzi.

Amezungumza hayo wakati wa mkutano mkuu wa CCM jimbo la Bukoba Vijijini katika uwasilishaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika kipindi cha miaka na amesema wanapokutana kwenye vikao vya pamoja waangalie changamoto mbalimbali na zitatuliwe.

Amesema, changamoto hizo zikikosa ufumbuzi wa kutatuliwa kwa Wananchi wanaweza kukata tamaa na cha hicho na kutowapitisha wagombea wa CCM kwenye kipindi cha uchaguzi na kikipatia chama hicho kazi kubwa ya kutumia nguvu nyingi ya kushinda wagombea.

Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Karimu Amri amewaasa wanachama wa chama hicho kwa mtu yeyote ambaye anayetafuta madaraka kwa misingi ya dini ua ukabira kwa kutumia wanachama wa chama cha mapinduzi wawapuuzwe.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini, Dkt. Jasson Rweikiza amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 walipata miradi 52 utengenezaji wa maeneo korofi ya barabara katika kata 29 zaidi ya shilingi bilioni 1.2 na mwaka 2021/2022 miradi 50 ya Barabara katika kata 29 ya utengenezaji kwa maeneo korofi.

Mingine ni karavati zaidi ya shilingi bilioni 2.06 na mwaka 2022/2023 walipata miradi 48 kwa ajiri ya kata 29 ilifanyiwa matengenezo maeneo korofi pamoja na karavati kiasi cha shilingi 1.9 ambapo Jimbo hilo la Bukoba vijijini ni moja kati ya majimbo mawili ya uchaguzi yakiwa na Tarafa nne, Kata 29, Vijiji 94 na Vitongoji 515 na jumla ya wakazi 322,448.

Mchengerwa ataka tathmini ya maboresho miundombinu ya Afya
Mogella: Simba SC wasahau kabisa ubingwa