Taharuki na maswali yamezidi kuibuka Nchini Slovakia bada ya Waziri Mkuu wa Taifa hilo, Robert Fico kupigwa risasi hapo jana Mei 15, 2024 na kujeruhiwa tumboni.

Fico alipatwa na mkasa huo muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye mji wa Handlova ulio kilometa 190 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bratislava na kukimbizwa hospitali kwa matibabu huku mshukiwa akikamatwa.

 

Baadhi ya raia, familia na Viongozi wa mataifa mbalimbali wameendelea kushangazwa na tukio hilo, ambapo mbali na kutoa salamu za pole bado wanajiuliza kisa hasa cha mshukiwa ambaye anaendelea kuhojiwa na vyombo vya usalama kutekeleza shambulio hilo.

Rais wa Slovakia, Zuzana Caputova amesema ameshtushwa na shambulio hilo na kumtakia Fico nafuu ya huku Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na marais wawili wa Umoja wa Ulaya wakilaani tukio hilo.

Simba SC mguu sawa Dodoma
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 16, 2024