Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ameiomba bodi ya Filamu Nchini kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kurusha mahudhui yanayofaa kwenye vituo vya Luninga, kwani kuna mapungufu na maudhui ya kichawi na kiganga yameshamiri.

Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara hiyo, Shabiby amesema Wizara na Bodi ya filamu wanatakiwa kuzingatia  jambo hilo kwani filamu ambazo zinatisha watu hazijengi wala kufundisha bali zinawaharibu waaribu watu kisaikolojia.

“Na sio watu wazima tu hata watoto wadogo wanaharibika kutokana na filamu hizo za kutisha, ni mnawaandaa watoto kuwa waganga wa kienyeji wa badaae kutokana na filamu zenu zisizofaa, ndiyo maana Watanzania wengi wanashinda mitandaoni kufuatilia umbea tu maana hata wakienda kutanzama televisheni hamna cha maana,” amesema Shabiby.

Waganga wa kienyeji: Serikali imetutenga utafiti wa maradhi sugu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 24, 2024