Sera ya Serikali ya kupiga marufuku elimu kwa Wanawake nchini Afghanistan, imekosolewa vikali na Kiongozi mkuu wa Taliban, Sher Abbas Stanikzai akisema huo ni ubinafsi na ni tafsiri ya sheria za Kiislamu.
Ni nadra kwa Sher Abbas kutoa karipio hadharani, na hii inakuja huku Mataifa yakiwataka watawala wa Afghanistan kuruhusu elimu kwa Wasichana pamoja na kuondoa vikwazo kwa Wanawake kimaisha.
Kundi la Taliban lilichukua utawala nchini Afghanistan mwaka 2021 na Kiongozi wao aliyejitenga, Hibatullah Akhundzada, ameanzisha tafsiri yake kali ya Sharia ya kutawala nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro.
Amri nyingi kimsingi zinazuia Wasichana kupata elimu zaidi ya darasa la sita na kuwakataza Wanawake kutoonekana katika maeneo ya kazi na maisha ya umma kwa ujumla.