Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imetangaza kufungwa kwa Barabara tisa za Jijini Dar es Salaam kwa siku sita kuanzia Januari 25 -30, 2025, ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27- 28, 2025, huku akielekeza kuwa bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.

Maisha: Ndugu zake wamemtuma aniwekee dawa
Uokoaji waendelea Rukwa miili mingine ikipatikana