Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi ameitupia lawama Jumuiya ya Kimataifa kwa kushindwa kufanya jambo lolote katika kukabiliana na mapigano ya mashariki mwa Taifa hilo.

Katika hotuba yake kwa Taifa usiku wa kuamkia hii leo Januari 30, 2025 kufuatia kutekwa kwa mji wa mashariki wa Goma, Tshisekedi amesema kuna hatari ya uwepo wa vita ya kikanda.

Amesema, “kimya chenu na kutochukua hatua ni tusi kwa DRC, kusonga mbele kwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda kunaweza kupelekea moja kwa moja vita katika ukanda wa Maziwa Makuu.”

Aidha, Tshisekedi ameongeza kuwa majibu yanapangwa na yapo njiani dhidi ya magaidi hao na wafadhili wao, huku akilalamikia hali ya usalama ilivyozorota eneo hilo la mashariki.

Hotuba ya Tshisekedi inakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya wapiganaji wa kundi la M23 kuteka Wilaya mbili katika jimbo la Kivu Kusini, huku hali ya usalama ikiwa si ya kuridhisha.

Bungeni: Miswada miwili marekebisho ya Sheria yapitishwa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 30, 2025