Kamati inayoshughulika na Hesabu za Serikali za Mitaa imesema katika kutekeleza majukumu yake ya kikanuni, Agosti na Oktoba, 2024 ilichambua taarifa ya Hesabu za Halmashauri 55 zilizokaguliwa, ambazo ni sawa na asilimia 29.89 ya Halmashauri zote 184.

Akisoma taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee amesema katika kipindi cha mwaka mzima kuanzia Februari, 2024 hadi Februari, 2025, Kamati ilikutana na kufanya mahojiano na jumla ya Halmashauri 69 na kufanya ziara za ukaguzi wa ufanisi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri 27.

Amesema, “jumla ya Halmashauri zote zilizofikiwa na Kamati ndani ya mwaka mmoja ni Halmashauri 96 sawa na Asilimia 52 ya
Halmashauri zote 184., 1.3 Ufuatiliaji wa Mapendekezo yaliyotolewa na Kamati.”

“Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Februari, 2024 Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliwasilisha Taarifa yake Bungeni kuhusu
shughuli za Kamati zilizotekelezwa kwa mwaka 2023 na Katika Taarifa hiyo, Jumla ya Mapendekezo Nane yalitolewa na baadae kuwa ni maazimio ya Bunge,” amesema Mdee.

Aidha, Mdee ameongeza kuwa Januari 14, 2025, Kamati ilikutana na CAG pamoja na Ofisi ya Raisi TAMISEMI, ili kupokea, kujadili na
kuchambua utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yanayotokana na Taarifa ya LAAC kwa kipindi cha Mwezi Februari, 2023 hadi Februari,
2024.

Hata hivyo, amesema azimio jingine lililotolewa katika eneo hili ni kuiyaka, Serikali ihakikishe gharama za usimamizi na ufuatiliaji wa
miradi zinajumuishwa katika fedha zinazopelekwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya force account, katika kila Halmashauri.

“Azimio hili pia limetekelezwa kwa Asilimia 80 ambapo, Serikali imewasilisha kwa CAG bajeti ya Shilingi Bilioni 8.6 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kugharamia usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri, kwa kiwango cha Shilingi Milioni 30 hadi 100 kwa kila Halmashauri,” alisema Mdee.

Amoeongeza kuwa pia Serikali iliwasilisha kwa
CAG taarifa ya kiasi cha Shilingi Bilioni 8.1 kilichotolewa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Disemba, 2024
Kwa ajili ya ufuatiliaji na tathmini kwa miradi yote.

Mdee amebainisha kuwa, azimio hilo limetekelezwa kwa asilimia 70 na Serikali iliajiri wataalamu wa kada ya Uhandisi, Wakadiriaji Majenzi, na Wasanifu Majengo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa miaka ya fedha 2021/22 na 2022/23.

“Bado kuna upungufu wa wataalamu hawa katika Halmashauri kama
ilivyoainishwa katika taarifa ya Kamati, Kuhusu Kutofanyika kwa Tathmini ya Mahitaji ya
Miundombinu Muhimu kabla ya Utekelezaji wa Mradi,” alisema.

“Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Azimio hili unaendelea na umefikia Asilimia 70 ambapo, Taarifa ya tathmini iliyowasilishwa kwa CAG kwa ajili uhakiki imebaini uwepo wa miradi 20 yenye thamani ya Shilingi 7.5 Bilioni katika sekta za Elimu na Afya ambayo haitumiki kutokana na changamoto za ukosefu wa umeme, maji, na Barabara ambapo changamoto hizo zinatarajiwa kutatuliwa kati ya Mwezi Januari hadi Juni, 2025,” amesema Mdee

Picha:Hivi ndivyo utakavyokuwa uwanja wa mpira Dodoma