Shirika la umeme Nchini (TANESCO), imeendelea kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji Makambako-Songea kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden.
Akizungumza hayo na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba leo Febuari 27,2025 Jijini Dodoma,ambapo amesema mradi huo umeanza tangu 2017 hadi sasa ambapo unakaribia kukamilika.
“Kuna miradi mbalimbali kama Bwawa la Mtera limepata mchango mkubwa sana kutoka Serikali ya Sweden kuna mikopo ambayo tumepatiwa kupitia wao”,amesema
“Alafu pia kuna miradi mingine ya Sola ambapo mikoa mingi imenufaika na mradi huo miaka ya nyuma na imesaidia sana kupata umeme kabla miradi ya umeme haijaanza kufika. Amesema Mhandisi Mramba.
Hata hivyo amesema Sweden wamekuwa wakishirikiana nao kwa karibu na miradi ya umeme ambayo inaendelea kutekelezwa.
“ Sweden ni Watu walioendelea sana katika masuala ya Nishati, na miradi yetu mingi tuliyoifanya ya umeme ni wao tumeshirikiana nao, na wanauzoefu mkubwa katika maeneo haya”, amesema
“Baada ya kukamilika kwa mradi huu wa Makambako-Songea huu umeenda mpaka mbinga hadi nyasa na sasa hivi tunaendelea kuusogeza zaidi kwenda mpaka tunduru, Maasasi hadi lindi, kwaio ni mradi ambao umefikia watu wengi na jumla ya vijiji ni 120,” qmesema Mhandisi Mramba.