Mohanmmed Iqbal Dar (80), ambaye alibuni jina la Taifa la TANZANIA, ameaga dunia katika jiji la Birmingham lililopo Nchini Uingereza alikokuwa akiishi.
Iqbal Dar aliyezaliwa Agosti 8, 1944, jijini Tanga, alikuwa mtoto wa Dkt. Tufail Ahmad Dar, daktari maarufu aliyehudumu nchini ambapo mwaka 1965 alihamia Uingereza.
Alishiriki katika shindano la kutafuta jina la Tanzania lililoandaliwa mwaka 1964 kabla ya Muungano ambako yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 na yeye kuibuka mshindi akiwa na miaka 18 ambapo alipatiwa zawadi ya Shilingi 200.
Enzi za uhai wake, Iqbal alisema alichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha nikaunganisha nikapata jina TANZAN.
Anasema baadaye alichukua herufi ya kwanza ya jina lake ‘lqbal’ kisha akachukua herufi ya kwanza A ya jina la dini yake yaani Ahmadiya na kuunda jina TANZANIA.