Johansen Buberwa – Kagera.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi – UVCCM, Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan amewaambua Vijana kuwa Mitaa haitaki Digree wala PhD ili mtu aonekane Kijana mchapa kazi.

Kauli hiyo ameitoa Machi 12, 2025 Wilayani Karagwe, wakati akizungumza na Vijana wa chuo hicho kuhusu umuhimu wa elimu ya Ufundi Stadi, wakati wa ziara ya Kamati ya utekelezaji ya UVCCM.

Amesema, “Nchi imewekeza kwenye viwanda na wanaofanya kazi kwenye mitambo siyo watu wenye masters na niwatu wenye elimu maarifa na ufundi niwaombe vijana kusoma kwa bidii ili elimu ya ufindi muifanyie kazi kulingana na fani mlizosomea bila kujali ukubwa wa elimu ya watu waliyowazunguka.”

Faris, amesema kwasasa Elimu ya ufundi ndiyo kimbilio kwa vijana hakuna haja kwa wale waliyopo vyuo vya kati na ufundi stadi kujitizama kinyonge niwakati wa vijana wanaosoma kozi za ufundi katika vyuo vya veta kujiona kama mashujaa wanaolipigania Taifa.

Chuo hicho kina wanafunzi 336 na nikati ya vyuo vya Veta hapa nchini ambavyo Serikali imewekeza fedha kuendeleza na kukarabati miundombinu ambapo Sh4.6 bilioni zimetumika kukarabati madarasa na kununulia vifaa vya kujifunzia.

Kapinga azindua namba ya bure Huduma kwa Wateja wa TANESCO