Johansen Buberwa – Kagera.
Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania JWT Mkoa wa Kagera wameanza mkakati wa kubadilisha changamoto kuwa furusa kwa Wafanyabiashara wa mkoa huo, ikiwemo kuchagiza urasimishaji wa biashara zao hali itakayosaidia kuwaondolea vikwazo vya kuvutana na mamlaka za kiserikali.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiasha Mkoa huo, Nicolaus Basimaki akizungumza katika ufunguzi wa Warsha hiyo ambayo imefanyika kwa muda wa siku tatu ndani ya manispaa ya Bukoba, ambayo imeshirikisha wadau mbalimbali zikiwemo Benk na wadau maendeleo amesema mpango huo utaongeza furusa za ulipaji wa ushuru na maombi kuongezeka pamoja na kufanya biashara za kisasa.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa Kagera, Castro John.
“Sisi katika utafiti wetu tulioufanya kama JWT tumeona inawezekana kulipa kodi pasipo kuvutana na kusumbuana kwa kuumizana,” amesema Basimaki.
Awali akizungumza kwenye warsha hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kagera, Castro John amesema JWT imekuwa na mchango mkubwa wa kuwaunganisha mamlaka hiyo na wafanyabiashara ambapo kuanzia mwezi Julia hadi February ilikuwa na mpango wa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 108 na imefanikiwa kukusanya bilioni 122.6 ikiwa imezidi kiwango cha asilimia 100.

Baadhi ya Washiriki na Wafanyabiashara wakiwa katika warsha hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha maji Bunena, Chikambi Rumisha amesema mkoa huo kijografia unapakana na Nchi tatu za ukanda wa Afrika Mshariki ambazo zingekuwa furusa ya wafanyabiashara hao kufanikiwa.
Aidha amesema baadhi ya biashara hazijakizi viwango vya kuwa biashara kubwa badala yake inaonekana kama uchuhuzi wadogowadogo inawabidi kupambana, ili kuwa na biashara kubwa hali itakayosadia kutovutana na mamlaka za kiserikali.

Katibu Tawala Mkoa Kagera, Stephen Ndaki.
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Stephen Ndaki ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye warsha hiyo amepongeza Jumuiya hiyo kwa kuja na mpango mzuri wa kuandaa bajeti ya muda wa miaka mitatu ambayo itatoa dira ya kuwa na uelekeo chanya kwa kuongeza wigo wa ulipaji kodi.
Amesema, Mkoa huo kwa miaka ya 70 ulikuwa unashika nafasi ya pili kitaifa na kuwataka Wafanyabiashara wa mkoa huo kuongeza ushirikiano na mshikamano iliwaweze kufanya uwekezaji katika biashara kubwa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiasha (JWT) Mkoa Kagera, Nicholaus Basimaki.