Waziri wa Madini, Anthony Mavunde leo Aprili 9, 2025 amefanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Marvel Gold, Timothy Strong juu ya uwekezaji wa kampuni hiyo kwenye sekta ya madini.

Kampuni hiyo kutoka nchini Australia imefika kujitambulisha na kuelezea mpango wao wa kuanzisha mgodi mkubwa wa dhahabu katika Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara.

“Tumeichagua Tanzania kwasababu ni nchi ambayo ina amani na usalama na mazingira mazuri ya uwekezaji,na tumevutiwa na mpango mzuri wa Rais Dkt. Samia S. Hassan kuvutia uwekezaji nchini Tanzania,” amesema Strong.

Ameongeza kwamba, kampuni hiyo itafanya utafiti wa kina kwa kurusha ndege na baadaye kukamilisha hatua zote za utafiti wa madini.

Ameeleza kuwa, kampuni hiyo inategemea kuanza zoezi la utafiti wa kina ifikapo mwezi Septemba 2025.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mavunde amewapongeza wadau hao kwa kuichagua Tanzania kufanya uwekezaji wao na kuwahakikishia kwamba serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha miradi kama hiyo yenye dhamira ya kukuza sekta ya madini inafanikiwa.

“Ninapokea watu wengi sana wenye nia kama ya kwenu, asilimia kubwa si wakweli kutekeleza mipango yao na wamekuwa na maneno mengi kuliko vitendo,” amesema Waziri Mavunde.

Kapinga: Vitongoji 9,000 kusambaziwa umeme 2025/2026
Lissu alegeza masharti CHADEMA kushiriki uchaguzi Mkuu