Wafanyabiashara wa Majokofu Mkoa wa Pwani, sasa wamepata unafuu wa bidhaa hiyo baada ya kiwanda cha Snowsea kilichoko Kwala kuanza uzalishaji wa vifaa hivyo na kuwauzia kwa bei rafiki.

Awali kabla ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji wafanyabiashara hao walikua wakilazimika kufuata bidhaa hizo Jijini Daresalaam hali inayoelezwa kuwa ilikuwa inawaongezea gharama na kushuka kiuchumi.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano April 9,2025 na baadhi ya wafanyabiashara hao muda mfupi baada ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha vifaa hivyo cha Snowc kilichoko Kwala Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Wakizungumza baada ya uzinduzi wa kiwanda hicho uliozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru wamesema kuwa hatua hiyo itawainua kiuchumi na kuvhangia maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

“Tumesogezewa bidhaa hatua hii si kuwa itatunufaisha sisi wafanyabiashara pekee bali hata wateja wetu pia watanufaika na serikali yetu hasa kwa upande wa kodi”amesema Mussa Samson.

Kwa upade wake Neema Jackson amesema kuwa awali walikuwa wakipata changamoto kubwa ya kufuata bidhaa hiyo Jijini Daresalaam hali ambayo ilikuwa inachangia kushuka kwa kipato.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ismail All Ussi amesema kuwa uwepo wa wawekezaji nchini unachangia kuchochea maendeleo kwa nyanja mbalimbali.

“Serikali imeweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ili kuchochea uchumi kwa nyanja mbalimbali ikiwemo kupitia ajira kwa wananchi hata ukusanyaji wa mapato kupitia kodi”amesema.

Kiongozi huyo amewataka Vijana wanaopta nafasi za ajira kwenye viwanda hivyo kufanyakazi kwa bidii na uaminifu ili kulinda heshima ya nchi na wao kuendelea kunufaika kwa kipato halali.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema kuwa Mkoa huo umeendelea kutekeleza kwa vitenda sera ya uwekezaji kwa kutenga maeneo makubwa ya ardhi ili kurahisisha uwekezaji hasa wa viwanda.

Afisa uzalishaji wa Kiwanda hicho Peter Abdalah amesema kuwa mpaka sasa wametoa ajira kwa Vijana 40 ikiwa ni hatua za awali na wanatarajia kufanya ongezeko kadri mahitaji yatakavyoongezeka.

Mwisho

Polisi Jamii watakiwa kuacha tabia ya kuwapiga raia
SOUWASA yawapa Tabasamu la Maji Wakazi wa Londoni