Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hii leo Aprili 11, 2025 amezungumza na Mmiliki wa Klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe.

Mazungumzo hayo, yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Kwa upande wake Six Rivers, Sir Jim Ratcliffe amesema Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 12, 2025
Wafanyabiashara wa Mifugo wapata soko la uhakika Pwani