Vyama 18 vya siasa ikiwemo CCM na ACT Wazalendo vimeshiriki utiaji saini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Udiwani unaotarajiwa kufanyika Okctoba, 2025 huku chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikisusia zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amesema CHADEMA walipata taarifa ya zoezi hilo kupitia kwa mkurugenzi wa Tume hiyo Ramadhan Kailima ambaye aliwasiliana na Katibu mkuu wa Chama hicho John Mnyika na kumueleza kuwa hawatoshiriki.
Katika itifaki ya kuketi kwenye zoezi hilo lililofanyika katika ofisi za makao makuu ya Tume eneo la Njendengwa jijini Dodoma katibu mkuu wa CHADEMA alipangwa kuketi kati ya kiti cha katibu mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi na Katibu mkuu wa CHAUMA Mohamed Rashid.
Vyama vilivyoshiriki ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU, UPDP, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK na UDP.