Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zimesainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima.

Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU, UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.

UCSAF kuboresha huduma za Mawasiliano Kilimanjaro
Kanuni za Maadili: Vyama 18 vyasaini makubaliano