Naibu Katibu Mkuu anayeshugulikia Afya OR-TAMISEMI Dr. Grace Magembe, amesema mpaka sasa Wananchi waliojiunga na bima ya Afya Tanzania ni asilimia 14 tu huku asilimia 86 ya Watanzania wakiwa wanalipia huduma za matibabu kwa kutoa hela mfukoni pale wanapougua.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Jijini Arusha Dk. Grace amesema haijalishi unajiunga na Bima gani cha msingi kila Mwananchi anatakiwa awe na bima ya afya.

Dk. Grace amesema hii maana yake ni kwamba Watanzania wanapata changamoto pale ambapo wanapata maradhi na wakati huo hawana fedha mfukoni au hawapati huduma stahiki kwasababu hawana fedha ya kutosha kupata huduma hiyo kwa muda huo lakini pia Wananchi hao mara nyingi wanapata changamoto ya kuingia katika umasikini kwa sababu ya kugharamia matibabu kila wanapougua.

Aidha, Dk. Grace amesema tathmini ya haraka inaonesha watu wengi hawana uelewa wa masuala ya bima ya afya lakini wengi wao wana uwezo wa kulipa na kufuatia hali hiyo amezitaka Kamati za Afya Mikoa na Wilaya (RHMT&CHMT) kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika kila ngazi ili kuwafikia Wananchi wengi zaidi kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ya afya.

Florent Ibenge afunguka maisha ya Clatous Chama
Zifahamu sababu za Morrison, Sakho kukosa mchezo wa kirafiki