Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Pyramids FC ya Misri umetuma malalamiko kwenda Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF ukigomea kitendo cha Yanga kubadilisha uwanja wa kuchezea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kufuatia mabadiliko ya uwanja huo, Pyramids  wameamua kutafuta sabubu rasmi zilizopelekea mabadiiko hayo kwa kutuma malalamiko yao CAF kwani wameonesha kutoa afikiana na maamuzi hayo.

Taarifa zinasema Pyramids wanaona kama ni mbinu za Yanga kuwapoteza kwenye mechi hiyo mpaka imefikia hatua ya kuhoji CAF.

 

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi hiyo ya ‘Play Off’ ambapo mshindi atafuzu mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Yanga ‘itamenyana’ na Pyramids Oktoba 27 kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza ambao awali ilifahamika mtanange huo  utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini baadaye Yanga wakaamua ichezewe Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.

Wanafunzi watano wafa maji Morogoro
Miaka minne ya kifo cha Filikunjombe, ibada maalumu yafanyika Ludewa