Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, amepiga marufuku sherehe za wanafunzi wanaohitimu darasa la 7, zinazofanywa na wazazi nyumbani, badala yake amesema itafanyika sherehe moja tu, katika Shule husika na kuwajumuisha ndugu wote.
Mtatiro amesema kuwa sherehe za kuwapongeza wanafunzi wanapohitimu darasa la 7, zinazofanywa na wazazi mbali na sherehe zinazofanywa na Shule, zimekuwa zikichangia wazazi wengi kushindwa kuwasomesha watoto wao pindi wanapofanikiwa kuingia kidato cha kwanza.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mtatiro amendika kuwa, “tofauti na maeneo mengi ya Nchi yetu, Tunduru kuna herehe 2 za kuwaaga darasa la saba, ya kwanza ni mahafali yanayoandaliwa na shule yakiwashirikisha wahitimu, wazazi wao na wanafunzi, haya ni Mahafali sahihi na hufanyika kabla ya mitihani ya darasa la 7”.
Mwaka huu 2020, kila Shule ya Msingi itafanya mahafali moja tu ambayo ni rasmi na itawahusisha wazazi, Walimu, Wahitimu, wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki, ile mahafali ya pili ambayo hufanywa na wazazi peke yao kwa kuwafuata watoto wao shuleni wakiwa kwenye vyumba vya mtihani wa mwisho, na kutumia gharama nyingi kufurahia kutua mzigo, tumeipiga marufuku na haitafanyika tena”. amesisitiza DC Mtatiro.
Aidha, Mtatiro ameeleza kuwa Wanafunzi wote waliomaliza Darasa la Saba Wilayani humo, wamefaulu na kukidhi sifa za kujiunga na Kitado cha Kwanza na atahikikisha wanajiunga na shule