Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema jeshi la polisi mkoani humo litaanza msako wa kuwabaini watu wanaotaka kujinyonga kufuatia kupokea taarifa ya watu kujinyonga.

Kamanda Mwakalukwa amesema kufuatia kupokea taarifa ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga.

Hata hivyo amewakanya watu wanaotegemea kujinyonga kuwa tabia hizo zikome kwani wao wataanza kufanya doria na kuwakamata kabla hawajajinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani.

“Tunaomba viongozi wa Taasisi za Kiroho wafanye doria za Kiroho za kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha, elimu na Wataalamu wa Afya waende kwa wagonjwa wenye matatizo ya akili ili wawape faraja kuwa bado wana nafasi ya kuwa na maisha bora.” amesema kamanda Mwakalukwa.

Ameongeza kuwa wakati mwingine tunapoteza Wataalamu ambao wangesaidia nchi yetu “Tumepoteza Mwalimu, Mjasiriamali labda hawa baada ya miaka miwili wangekuwa Maprofesa au matajiri wa Afrika.”

Gugu tishio Afrika latua Arusha na kuua Mifugo
Video: Mapya yaibuka mtoto aliyeibwa na kichaa Mbeya, Bibi afunguka 'Watoto kuuzwa'