Mwenyekiti wa kamati ya usajili Young Africans Dominic Albanus amesema ni vyema wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wakasubiri dirisha la usajili litakapofunguliwa kufahamu nyota watakaosajiliwa.

Dominic amewataka mashabiki na wanachama wa klabu Young Africans kuwa na subra kufuatia siku za karibuni idadi kubwa ya wachezaji kuhusishwa na klabu yao.

Amesema mpaka sasa Young Africans imehusishwa kutaka kuwasajili zaidi ya wachezaji 30 jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani.

“Mimi sijui hizi taarifa zinatoka wapi kwa sababu kama timu bado hatujaanza michakato ya usajili kwa sababu dirisha la usajili bado halijafunguliwa,” amesema

“Inawezekana kutokana na janga la corona, shughuli zote za michezo zimesitishwa hivyo waandishi wa habari wanalazimika kutengeneza habari.”

Dominic ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa Young Africans imeanza mawasiliano na beki wa zamani wa Simba Juuko Murshid kwa ajili ya kumsajili.

“Hatujawahi kuwasiliana na Juuko, kwanza hatufahamu hata alipo. Kwa kweli tunashangaa habari hizi zinatokea wapi?”

Dominic amesema dirisha la usajili litakapofunguliwa watahakikisha wanaunda kikosi imara kwa kufuata mapendekezo ya kocha Luc Eymael.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Young Africans Dominic Albanus amesema ni vyema wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wakasubiri dirisha la usajili litakapofunguliwa kufahamu nyota watakaosajiliwa.

Dominic amewataka mashabiki na wanachama wa klabu Young Africans kuwa na subra kufuatia siku za karibuni idadi kubwa ya wachezaji kuhusishwa na klabu yao.

Amesema mpaka sasa Young Africans imehusishwa kutaka kuwasajili zaidi ya wachezaji 30 jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani.

“Mimi sijui hizi taarifa zinatoka wapi kwa sababu kama timu bado hatujaanza michakato ya usajili kwa sababu dirisha la usajili bado halijafunguliwa,” amesema

“Inawezekana kutokana na janga la corona, shughuli zote za michezo zimesitishwa hivyo waandishi wa habari wanalazimika kutengeneza habari.”

Dominic ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa Young Africans imeanza mawasiliano na beki wa zamani wa Simba Juuko Murshidi kwa ajili ya kumsajili.

“Hatujawahi kuwasiliana na Juuko, kwanza hatufahamu hata alipo. Kwa kweli tunashangaa habari hizi zinatokea wapi?”

Dominic amesema dirisha la usajili litakapofunguliwa watahakikisha wanaunda kikosi imara kwa kufuata mapendekezo ya kocha Luc Eymael.

“Tumedhamiria kuunda kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao tuweze kurejesha utamaduni wa kushinda mataji. Mashabiki wetu wawe na subira, tunawahakikishia yajayo yanafurahisha.”

Corona: Mbowe wa Chadema kutohudhuria vikao vya Bunge
JPM atoa wito kwa waajiri siku ya wafanyakazi