Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametoa taarifa kuwa wameafikiana na wabunge wote wa chama hicho kutohudhuria vikao vya Bunge, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya corona.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho inaeleza kuwa mara kadhaa wameshauri kuchukuliwa hatua za dharura ili kupunguza kasi ya maambukizi ya covid 19, na sasa wameamua kuchukua hatua.

Wakati wanasubiri Serikali kuchukua hatua hizo wao wamefikia uamuzi kwamba wabunge wote wa Chadema waache mara moja kuhudhuria vikao au Kamati za Bunge na kutofika kabisa katika eneo la Bunge jijini Dodoma .

Wabunge hao watajiweka karantini kwa muda usiopungua wiki 2, kwa wabunge walioko Dodoma wametakiwa wasiende majimboni kwao hadi itakapothibitika hawana maambukizi ya virusi vya corona.

Aidha wamelitaka Bunge kusitisha shughuli kwa siku 21 ili kuwapima Wabunge, Watumishi wa Bunge na familia zao kama wana maambukizi.

Shule kufunguliwa Septemba, amri ya corona yalegezwa – Rwanda
Young Africans yamkana Juuko Murshid