Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir ameunda Bunge jipya ambalo lina Wabunge 550 kama walivyokubaliana katika makubaliano ya awali Septemba 2018 ambayo pia yalitaka 35% ya viti kupewa Wanawake.
Wabunge waliotangazwa wanajumuisha Wabunge 128 kutoka Kundi la Waasi wa zamani toka SPLM-IO wanaoongozwa na Makamu wa Rais wa kwanza Riek Machar na 332 kutoka SPLM.
Vilevile, Chama cha South Sudan’s Opposition Alliance (SSOA) kitakuwa na viti 50, vyama vingine viti 30 na Wafungwa wa zamani viti 10.
Kwa mujibu wa makubaliano ya amani, vyama mbalimbali vilitakiwa kuchagua wawakilishi wao ili waweze kuteuliwa na Rais.