Serikali ya Marekani imepitisha sheria ya dharura siku ya Jumapili baada ya bomba kubwa la mafuta la nchini humo kushambuliwa kimtandao na genge la wahalifu linalotaka malipo.

Bomba hilo kwa jina la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku sawa na 45 ya mahitaji ya mafuta ya Pwani ya Mashariki ya nchi hiyo na linasambaza mafuta ya dizeli, ya petroli na mafuta ya ndege.

Wahalifu wa mtandaoni walifanya hujuma dhidi ya bomba hilo ambalo limeshindwa kufanya kazi tangu siku ya Ijumaa na mpaka sasa bado oparesheni ya kujaribu kurudisha huduma za bomba hilo zinaendelea.

Hata hivyo hali ya dharura inaruhusu mafuta kusafirishwa kwa njia ya barabara.

Jumla ya majimbo 18 yamepewa muda kidogo kusafirisha mafuta ya petroli, dizeli, ya ndege na aina nyingine za bidhaa za mafuta.

Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Columbia, Delaware, Florida, Georgia, Kentucky, Louisiana, Maryland, Mississippi, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, South Carolina, Tennessee, Texas na Virginia.

Wataaamu wanasema bei ya mafuta inaweza kuongezeka kwa asilimia mbili mpaka tatu leo Jumatatu, lakini athari zitakuwa kubwa zaidi kama tatizo hili litaendelea zaidi ya Jumatatu.

Mchambuzi huru wa soko la mafuta Gaurav Sharma ameiambia BBC kuwa kuna shehena kubwa ya mafuta iliyokwama kwenye vituo vya kusafishia mafuta huko Texas.

“Labda kama wataweza kutatua tatizo hilo ifikapo Jumanne, ila wapo kwenye tatizo kubwa,” amesema Sharma.

Sharma ameeleza kuwa maeneo ya kwanza ambayo yatapata athari yanaweza kuwa ni Atlanta na Tennessee, na athari inaweza kufika New York.

Nchi Saba kushiriki maonyesho ya sabasaba
Waliotoka jela kwa msamaha wa Rais Samia wauawa