Kesi ya ufisadi dhidi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imeanza leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.
Kiongozi huyo ambaye aliwahi kusherehekewa kwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.
Aidha Zuma amesema kuwa yeye ni mwathiriwa wa hujuma za kisiasa na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa.
Hata hivyo Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.
Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini walio hai wamemshtumu Rais huyo kumlinganisha na jambazi na kuonya kuwa huenda itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.
Mrithi wake, Cyril Ramaphosa, aliingia madarakani kwa kuahidi kutatua tatizo hilo, raia wa Afrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.