Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro Mei 27, 2021 kwa ziara ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atapata fursa ya kushiriki mdahalo na kufunga maadhimisho ya wiki ya kumbukizi ya Hayati Sokoine, yanayofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka wanachi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika shughuli hiyo.

Makamu Mkuu wa chuo SUA Profesa Raphael Chibunda amesema wananchi watapata fursa ya kupata elimu ya ujuzi mbalimbali ikiwemo kilimo bora.

Hayati Sokoine alifariki Aprili 12 mwaka 1984 kwa ajali ya gari wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambapo maadhimisho hayo hayakufanyika Aprili mwaka huu.

Kunenge azungumza na wakulima pwani
Kesi ya Zuma dhidi ya rushwa yaanza