Siku moja kabla ya kilele cha Siku ya Mazingira duniani, Serikali imezindua Mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa mwaka 2021 hadi 2026.

Mpango huo umezinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo leo jijini Dodoma ambapo amewataka wananchi kuishi kwa kufuata misingi ya ajenda za kimazingira.

Aidha katika uzinduzi wa Mpango huo, Waziri Jafo pia amefungua kongamano la hifadhi ya mazingira na maendeleo endelevu na kusema kuwa mkakati huo utasaidia kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Hata hivyo Waziri Jafo amesisitiza jukumu la kulinda mazingira kwa kila mwananchi.

“Bila kulinda mazingira hapa duniani siyo sehemu salama hivyo kuna kuna haja kwa Nchi zilizoendelea kusaidia Nchi maskini kupamban na athari za kimazingira zinazosababishwa na tabia nchi,” Amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema kuwa zaidi ya watu Milioni 1.6 wa Ukanda wa Pwani watakabiliwa na changamoto za kimazingira ifikapo mwaka 2030 endapo jamii itaendelea na shughuli zake zinazoathiri mazingira.

Rais Samia akubali chanjo ya corona
IGP Sirro apangua Makamanda, ACP Magiligimba ahamishiwa Ilala