Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekosoa vikali shambulizi lilifanywa dhidi ya Jenerali Katumba Wamala. 

Katika taarifa aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Museveni amesema amezungumza mara mbili na Katumba kwa njia ya simu akiongeza kuwa jenerali huyo anatibiwa vizuri na wameshapata taarifa za awali kuhusu wauwaji.

 Aidha, Museveni amesema mlinzi wa Katumba alifyatua risasi kuwaonya washambuliaji hatua iliyoyaokoa maisha ya jenerali huyo lakini alitakiwa kuwapiga risasi na kuwauwa. 

Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Flavia Byekwaso amesema watu waliojihami kwa silaha wamelimiminia risasi gari lililokuwa limembeba waziri wa Uganda katika tukio linalosemekana kuwa la jaribio la kumuua. 

Shambulio hilo limemjeruhi mkuu huyo wa zamani wa majeshi nchini Uganda, na kusababisha kifo cha mtoto wake wa kike na dereva wake.

Ajali ya basi la Classic yaua watatu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 2, 2021