Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewahasa wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona.

Ameyasema hayo leo Juni 1, 2021 mkoani Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, ambapo pia ametoa mashuka 200 yatakayotumiwa na wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na Watumishi wa hospitali hiyo, Rais Samia amewataka kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia Wananchi na kuwapatia huduma stahiki.

Aidha, Rais Samia ameahidi kuwa Serikali itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi hao, pindi hali ya uchumi wa Taifa itakapokuwa nzuri na kushughulikia changamoto ya upungufu wa dawa kufuatia malalamiko aliyopatiwa na wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo.

Kocha Gomes afichua siri Simba SC
Young Africans yabisha hodi KMC FC