Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasimamisha kazi uongozi wote wa soko la Kariakoo leo Juni 1, 2021 kutokana na hali mbaya aliyoikuta sokoni hapo alipofanya ziara ya kushtukiza.

Aidha, Rais Samia ameviagiza vyombo vya serikali vya usalama kufanya uchunguzi kwa uongozi huo, amesema lengo la serikali ni kusaidia wafanyabiashara.

Kutokana na hali aliyoikuta sokoni hapo, Rais Samia amesema serikali itafanya tathmini ya uendeshaji wa soko hilo ili kuona kama soko hili liongozwe na jiji au uongozi wa soko ili wafanyabiashara hao waweze kupata faida hata wanapoingiza bidhaa zao kwa kuwa na mpango mzuri.

Sambamba na hayo, Rais samia amewaasa wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara zao kwa kufua sheria na taratibu za nchi zinawekwa katika maeneo husika huku serikali ikiendelea kupanga njia nzuri ya kuwapanga wafanyabiashara hao

“Kwasababu nimeona njia zote zimezingilwa vibanda kila mahali kwaiyo nitakaa na uongozi wa jiji tuone njia nzuri ya kuwapanga,” amesema Rais Samia.

Mbunge atolewa Bungeni kisa mavazi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni Mosi, 2021