Watu watatu wamefariki dunia huku wengine wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Classic kupata ajali eneo la Buyubi kata ya Didia barabara ya Kahama – Tinde Halmashauri ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, Juni 2, 2021, majira ya 10 alfajiri ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Jijini Kampala nchini Uganda kuelekea Jijini Dar es salaam.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya majeruhi wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva kushindwa kuimudu kona ya Didia.

Aidha jeshi la Polisi wilayani Shinyanga limefika mapema eneo la tulio na kuimarisha ulinzi.

Kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema kuwa kwa sasa juhudi zinazofayika ni kulinyanyua basi hilo ili kubaini idadi kamili ya waliopoteza maisha.

Majaliwa awataka Makatibu Tawala kuhakikisha miradi inawafikia wananchi
Museveni alaani shambulio dhidi ya Jenerali Katumba