Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro leo Juni 4,2021 amefanya mabadiliko ya Makamanda watatu wa Polisi wa Mikoa ya Ilala, Shinyanga na Songwe.

Katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora Magiligimba aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga amehamishiwa Mkoa wa Kipolisi Ilala Kanda Maalumu ya Dar es salaam, akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Janeth Magomi anayeenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), George Kyando aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Jafo na kishindo kingine kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Rais Samia aagana na Balozi wa China