Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara za Fedha na Mipango na TAMISEMI kuanza usimamizi wa ujenzi wa Soko Kuu la Kariakoo kwa kuwa Serikali imepata Fedha zaidi ya Bilioni 34.

Rais Samia ameyasema hayo leo tarehe 4 Novemba alipotembelea Fukwe za Coco Beach kwa ajili ya kusalimiana na wafanyabiashara wadogo waliopangwa na Serikali eneo hilo.

Rais Samia akizungumza na Wafanyabiashara wa Coco Beach

Katika mazungumzo hayo Rais Samia amesema Serikali inawajali wafanyabiashara wadogo na kuwashukuru wote walioondoka maeneo walitakiwa kutoka bila kuleta vurugu huku akiupongeza Uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kazi hiyo ya Unadhifu wa Jiji.

Aidha Rais Samia amesema Serikali kupitia TAMISEMI imeandaa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zitakuwa ni kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara wadogo.

Baada ya ziara ya Coco Beach Rais Samia alikwenda kumtembelea Makamu wa Rais Mstaafu Gharib Bilal Nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia akisalimiana na Dkt Mohamed Gharib Bilal

Matabibu mtarudia mitihani:Mganga Mkuu Sichalwe
Bilioni 1.6 kuchagiza ushindi wa Taifa Stars kombe la Dunia