Mamlaka za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimesema zitapiga marufuku Raia ambao hawajapata Chanjo dhidi ya COVID19 kusafiri nje.
Wote waliopata chanjo kikamilifu wanatakiwa kupata ya nyongeza ili kukidhi vigezo vya kusafiri.
Hata hivyo, marufuku hiyo itakayoanza Januari 10 italegezwa katika mazingira kadhaa ikiwemo yale ambayo Mamlaka zimesema ni ya kibinadamu, na pale Raia wanaposafiri kwa ajili ya matibabu.
Hatua hii inakuja ambapo kirusi cha Omicron kinaendelea kusambaa nchi nyingi na kwa haraka zaidi ambapo wengi zaidi wamelazwa.
Hata hivyo nchi nyingi zimeendelea kufunga mipaka kwa sababu ya Uviko 19 na katika wimbi hili la nne la Omicron bara la Ulaya na Amerika yameongoza kwa kufunga mipaka na safari za ndege za kimataifa.