Jumla ya watu 11 wamefariki huku kukiwa na idadi ya wagonjwa 43 wakiendelea kuumwa na ugonjwa ambao mpaka sasa haujajulikana katika mkoa wa Dodoma na Manyara idadi hiyo ni hadi kufikia julai 03  .

Ripoti kutoka Wizara ya Afya inasema kuwa Mikoa ya Dodoma na Manyara ndiyo iliyoripoti wagonjwa kutoka katika Halmashauri za Chemba (34), Kondoa nne, Dodoma Manispaa moja, Chamwino moja na Kiteto tatu huku vifo 10 viliripotiwa na halmashauri ya Chemba, na kifo kimoja na kutoka Kiteto.

Aidha ripoti hiyo imefafanua kuwa timu ya wataalamu kutoka sekta mbalimbali zimeshafika mikoa ya Manyara na Dodoma kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kwamba tayari sampuli za damu zimekwishapelekwa Marekani katika kituo Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Centres for Disease Control and Prevention – CDC)

Kama uchunguzi wa awali ulivyonyesha kuwa vyakula vilivyokuwa na sumu ya Kuvu ndio chanzo, Serikali imesema itaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuanzia ngazi ya taifa mpaka wilaya ili kuhakikisha nafaka zenye sumu ya kuvu kwa kiasi kisichokubaliwa hazitumiwa.

Hata hivyo ripoti hiyo imesisitiza kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi za uandaaji wa chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu (aflatoxin) kwa nafaka ambazo hazijaharibika sana hii ikiwa pamoja na kuchambua nafaka zilizoharibika(zilizooza kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuachakutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika sana.

 

Rafa Benitez: Inatosha, Hatoondoka Mwingine
Serena Na Venus Williams Wajisogeza Robo Fainali