Balozi mpya wa Marekani John Godfrey amewasili mjini Khartoum nchini Sudan baada ya kutokuwepo kwa mjumbe wa Marekani nchini humo kwa miaka 25 kutokana na tofauti za kidiplomasia ya pande hizo mbili.
Taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini Sudan imesema, “Godfrey aliwasili Khartoum kuwa balozi wa kwanza wa Marekani nchini Sudan takriban miaka 25, na kwamba hatua hiyo itaimarisha zaidi uhusiano wa Marekani na Sudan na kuunga mkono matarajio yao ya uhuru, amani, haki, na mpito wa kidemokrasia.”
Marekani, ilifunga ubalozi wake mwaka 1996 nchini Sudan baada ya kuutuhumu kwa kuwa mwenyeji wa marehemu kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden kitendo kilichosababisha kuzorotesha ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama tangu Oktoba 25.
Sudan, imekuwa katika wimbi la maandamano ya wananchi tangu Oktoba 25, 2021, wakidai kurejeshwa madarakani kwa utawala wa kiraia na wakikataa hatua zilizochukuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Kamanda wa Jeshi Abdelfattah al-Burhan, ambaye anatazamwa kama kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi.
Al-Burhan, amekuwa akipuuzia shutuma hizo akisisitiza kwamba hatua hizo zinalenga kurejesha mchakato wa awamu ya mpito na kuahidi kukabidhi madaraka kwa njia ya uchaguzi au makubaliano ya kitaifa.
Mwaka 1996, Washington iliamua kufunga ubalozi wake huko Khartoum, baada ya kuiweka Sudan kwenye orodha nyeusi ya nchi zinazofadhili ugaidi, kwa sababu ya mapokezi ya wakati huo kati ya Serikali ya Omar al-Bashir na Mwanzilishi wa shirika la Al Qaeda, Osama Bin. Laden, ambaye aliishi nchini humo kutoka 1992 hadi 1996.