Hali ya sintofahamu imezuka kuhusu iwapo Tume ya Uhuru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewezesha upatikanaji wa seva nane kama ilivyoagizwa na Mahakama ya Juu mnamo Jumanne, Agosti 30. 

Katika siku ya pili ya kusikilizwa kwa kesi ya kesi ya uchaguzi wa urais, Wakili Philip Murgor, anayemwakilisha Raila Odinga na Martha Karua wameiambia Mahakama kuwa IEBC bado haijawapa ufikiaji kamili wa seva hizo.

“Ningependa kuripoti kwamba kufikia asubuhi hakuna kilichobadilika, IEBC inaendelea kukataa kutoa picha ya uchunguzi wa seva zote 8. Kati ya seva hizo 8, IEBC imetoa ufikiaji mdogo tu kwa seva nambari 5,” amesema.

Mahakama kazini, Picha na Citizen Digital.

“Tulipokea ripoti kamili kutoka kwa timu yetu ya kiufundi iliyokuwa ikiongoza zoezi hilo IEBC na tumefahamishwa kuwa shughuli ya kuafiki sheria hiyo ilikamilishwa jana usiku.” amesema.

Mzozo ulishuhudiwa katika makao makuu ya IEBC wakati maafisa wa tume hiyo walipokataa kutoa ufikiaji wa seva zake kulingana na agizo la Mahakama ya Juu.

Wakili James Orengo, ambaye pia anawawakilisha Raila na Karua na kuiambia mahakama kuwa wameruhusiwa kufikia seva moja pekee.

Katika ripoti inayokinzana Jumatano jioni, IEBC ilisema imeruhusu wahusika kupata seva hizo.

“Kufuatia agizo la Mahakama ya Juu, IEBC imeruhusu wahusika kupata seva na zoezi la ukaguzi linaendelea,” ilisema taarifa kutoka tume hiyo.

Kenya: Raila hapaswi kuilaumu IEBC kufeli kwa Mawakala - Gumbo
Hassan Mwakinyo amfuata Liam Smith