Bondia Hassan Mwakinyo amesema hana budi kulipa kisasi dhidi ya Mpinzani wake Liam Smith, baada ya kupoteza pambano la Jumamosi (Septemb 03) mjini Liverpool kwa TKO.
Mwakinyo ametoa kauli hiyo kwa uchungu, akidai hakuridhishwa na maamuzi dhidi yake katika pambano hilo ambalo amedai alifanyiwa figisu za makusudi ili kumnufaisha Smith aliyekua nyumbani.
Amesema pamoja na kulalamikia baada ya matukio huku akiomba msaada wakati pambano likiendelea, Mwamuzi hakumsikiliza, hali ambayo imempa hasira na kujiapiza lazima alipe kisasi.
Bondia huyo kutoka Mjini Tanga baada ya kupata uhakika wa Pambano hilo kurudiwa mwezi Januari 2023, amehisi kufarijika na sasa ameanza kujiandaa ili kutimiza lengo la kulipa kisasi.
“Sikufanyiwa haki katika pambano la juzi, nimedhalilishwa vya kutosha dhidi ya mpinzani wangu, nitahakikisha ninalipa kisasi kwa ajili yangu na kwa watanzani wote.” amesema Mwakinyo
Kupitia Ukursa wake wa Instagram Bondia Hassan Mwakinyo amethibitisha taarifa za kurudiwa kwa Pambano lake na Liam Smith mwezi Januari 2023.
Mwakinyo ameandika: Kutokana na mchezo wa jana na kitendo cha refa ree kuwa unfair kwangu kime mlazimu promoter @benjshalom kutupa nafasi ya rematch na Liam Januar2023??