Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo za uwekezaji hapa nchini.

Profesa Ndalichako, amesema hayo hii leo Oktoba 22, 2022 jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la kitega uchumi la Mzizima Tower, linalomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea maendeleo ya mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower jijini Dar es Salaam, linalomilikiwa na NSSF.

Amesema, “Tunafahamu namna ambavyo Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan anafungua fursa za Uwekezaji, kwa hiyo nanyie NSSF mnatengeneza mazingira ambayo wawekezaji watakapokuja nchini watapata sehemu ya kuishi na sehemu ya kufanya biashara zao.”

Prof. Ndalichako amesema kupitia uwekezaji huo wa mradi wa Mzizima Tower inadhihirisha kuwa NSSF inaunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower lililopo jijini Dar es Salaam, linalomilikiwa na NSSF.

Aidha ameongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaendana na kazi kubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa anaifanya ya kufungua uchumi wa nchi, kuweka mazingira mazuri kwenye sekta binafsi na kukaribisha wawekezaji nchini.

Waziri huyo amezidi kufafanua kuwa, “Tumeshuhudia kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambavyo imefungua fursa na hivi sasa wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali wanakuja nchini, hivyo bado tunahitaji majengo mengi zaidi ya biashara ikiwemo hoteli ya namna hii.”

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, (hayupo pichani), mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower jijini Dar es Salaam, ambalo linamilikiwa na NSSF.

Hata hivyo, amewasihi NSSF kuendelea kufanya kazi kwa wakati ili Serikali iweze kuona manufaa ya mradi huo na fedha za wanachama ambazo zimewekezwa kupitia mradi huu zianze kurejeshwa ikiwemo kutengeneza ajira kwa vijana.

Ndalichako, pia ameipongeza Bodi ya Wadhamini, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na Managementi kwa kazi kubwa waliyoifanya, huku Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akisema maendeleo ya ujenzi wa mradi huo yanaendelea vizuri.

Msanifu Majengo, Kaisi Kalambo, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, (hayupo pichani) kuhusu maendeleo ya mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower jijini Dar es Salaam,w ambalo linamilikiwa na NSSF.

Awali, Msanifu wa Majengo ya Mzizima Tower, Kaisi Kalambo alimueleza Waziri Prof. Ndalichako kuwa maendeleo ya mradi huo yamefikia asilimia 88 na kwamba jengo hilo likikamilika litatumika kwa matumizi ya ofisi, hoteli na makazi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 23, 2022   
Askari 300 wapelekwa kuudhibiti moto mlima Kilimanjaro