Mtoto wa Miaka 10 kutoka kijiji cha Kakese, wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ameuwawa na watu ambao majina yao hayajatajwa wakati akiwa kuchunga ng’ombe.

Akiwa katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kakese kata ya Kakese, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24, 2022 wakati mtoto huyo akiwa machungani, ndipo alipokutana na watu hao kwa lengo la kuiba Ng’ombe wanne waliokuwa wakichungwa na Mtoto huyo.

“Pengine aliwatambua na wenyewe wakamtambua kwa hiyo wakaona ili kufanya namna gani iishe ni kufanya ukatili kwa kiumbe kile”

Hata hivyo,DC Jamila amesema Ng’ombe hao wamepatikana na wahusika wote wamekamatwa.

DC Jamila ametoa pole kwa familia iliyokumbwa na kadhia hiyo huku akiwaahidi wananchi kuwa serikali itaimarisha ulinzi na wote wanaovunja sheria watachukuliwa hatua.

Kilio kikubwa cha wananchi wa Kijiji hicho kwa serikali ni kuwajengea kituo cha Polisi kwani wanadai usalama kijijini hapo umekuwa mdogo kutokana na wizi kushamiri vikiwemo vitisho.

Ajali ya Moto yauwa Wanafunzi 11
Moses Phiri amtwisha zigo zito Clatous Chama