Hatimaye Wabunge nchini Marekani, wamemchagua Kevin McCarthy kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi huku kukiwa na majibizano makali ambayo yangeweza kuzua tafrani baina ya wawakilishi wa chama chake cha Republican.

McCarthy, ameshinda nafasi hiyo baada ya duru 15 za upigaji kura licha ya chama chake kuwa na kura nyingi katika bunge na ushindi wake umekuja baada ya kampeni kali ya shinikizo huku mmmoja wa waasi wa chama Matt Gaetz aliyekuwa hamuungi mkono mwanasiasa huyo akihimizwa kumpigia kura.

Spika mpya wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy. Picha ya Vox.

Awali, kulikuwa na majibizano makali na Gaetz alikuwa karibu apigwe na Mwakilishi Mike Rogers ambaye ni mfuasi wa McCarthy, Mbunge wa Alabama aliyezuiwa na wenzake wakati akimfokea na kumnyooshea kidole Gaetz.

Kwa taratibu za nchi ya Marekani Spika wa bunge huweka ajenda za Bunge na husimamia shughuli za kutunga sheria na nafasi hiyo ni ya pili kwa ukubwa nchini Marekani kama ilivyo kwa makamu wa Rais baada ya Rais wa Taifa hilo lenye nguvu Duniani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 8, 2023
Shule ya Dkt. Samia kupokea Wanafunzi 1,080