Maafisa wa Polisi jijini nchini Marekani, wamesema mwanafunzi mmoja (6), wa darasa la kwanza amempiga risasi na kumjeruhi mwalimu wake huko Virginia baada ya kutokea kwa ugomvi baina yao darasani.

Mkuu wa Polisi wa Newport News, Steve Drew amewaambia Wanahabari kuwa hali ya mwalimu huyo ilikuwa imeimarika kwa kiasi fulani kufikia majira ya alasiri, na Polisi walisema mtoto huyo alikuwa na bunduki darasani bila kugundulika.

Polisi wakiwa eneo la tukio. Picha ya Al Jazeera.

Katika tukio hilo, hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea katika Shule ya Msingi ya Richneck, na Polisi walisema Mwalimu huyo wa kike (30), alipata majeraha ya makubwa.

Mkuu huyo wa Polisi, hakujibu maswali kuhusu iwapo mamlaka ilikuwa inawasiliana na wazazi wa mtoto huyo, lakini akasema maafisa wa idara ya polisi walikuwa wakishughulikia uchunguzi juu ya tukio hilo.

Wanafunzi na Polisi walikusanyika nje ya Shule ya Msingi ya Richneck baada ya Mwalimu kupigwa risasi. Picha ya AP

Mwaka wa 2000, mvulana wa miaka sita akiwa na Bunduki alifyatua risasi ndani ya eneo la Buell Elementary karibu na Flint Michigan, na kumpiga mtoto mwingine wa miaka sita Kayla Rolland, shingoni, ambaye alikufa nusu saa baadaye.

Shule ya Dkt. Samia kupokea Wanafunzi 1,080
Dkt. Tax awataka Watumishi kuboresha utendaji