Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ni Katika sekta ya Kilimo nchini ni lazima kuweka mikakati ya kuboresha uzalishaji wa mazao yenye ubora ya kuanza kutafuta masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Bashe, ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Dar24 Media ofisini kwake jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mwandishi aliyetaka kufahamu namna Wizara inavyopambana katika utafutaji wa masoko kwa ajili ya mazao ya Wakulima.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Amesema, “huwezi kuwa darasa la saba kama hujapida darasaza la kwanza, mimi kama Waziri mtizamo wangu ni kuzalisha mazao bora halafu ndiyo soko lifuate, ni ubora kwanza lakini pia kuongeza tija ili gharama zangu za uzalishaji ziwe ndogo.”

Bashe ameongeza kuwa, ili mnunuzi aweze kulichukua zao la mkulima na kulichakata ni lazima akutane na bei nafuu, ambapo akiingia katika sokoni soko la ndani, nje au lile la ushindani awe na bidhaa bora na yenye gharama nafuu.

Anayedaiwa kuchakachua mbolea afungiwa Leseni
Robertinho: Tunatakiwa kuonesha ukubwa wetu