Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa muda wa wiki moja kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha inawasilisha vishikwambi vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya Walimu.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema ambaye pia amesema hatua hiyo inafuatia uwepo wa malalamiko ya kutotekelezwa kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji huo wa vishikwambi.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema.

Amesema, “ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi.”

Aidha, Mjema ameongeza kuwa chama kinaielekeza Wizara husika kuhakikisha zoezi hilo linakamilika na walengwa wote wanaostahili kupatiwa vishikwambi hivyo wawe wamepata.

TFS kuelimisha jamii umuhimu miradi ya ufugaji wa nyuki
Maporomoko ya theluji: Idadi ya waliofariki yafikia 28