Maelfu ya waandamanaji nchini Peru, wameandamana katika mji mkuu Lima, wakitaka rais Dina Boluarte aondolewe madarakani kufuatia kuwekwa kizuizini kwa Rais wa awali Eduardo Castillo.

Waandamanaji hao, walikabiliana na Polisi waliotumia gesi ya machozi na moshi ili kuwakabili huku wengi wao wakitokea vijiji vya maeneo ya Andean ambako watu 55 waliuwawa kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya rais wa kwanza kutokea eneo lao, Eduardo Castillo kuondolewa madarakani.

Baadhi ya Waandamanaji, ambao wanadaiwa walikabiliana na Polisi nchini Peru. Picha ya Wikipedia.

Castillo, amewekwa kizuizini na anatarajiwa kushtakiwa kwa uasi baada ya kuondolewa kwa nguvu madarakani na Peru inashuhudia machafuko mabaya ya kisiasa ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.

Hata hivyo, Rais wa Peru, Dina Boluarte Januari 14, 2023 aliomba radhi kwa makumi ya vifo katika maandamano ambayo yalizuka kote nchini humo, lakini akasisitiza kwamba hatajiuzulu.

Aliyepanda juu ya nguzo za umeme ahojiwa na Polisi
Waziri Nape akagua ujenzi ofisi ya Wizara