Ujenzi wa jengo la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari unatarajiwa kukamilika Oktoba 2023 hivyo kuongeza ufanisi wa wizara hiyo katika kuwahudumia Watanzania.

Akizungumza leo jijini Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo linalojengwa katika Mji wa Serikali – Mtumba, Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye amesema atatoa ushirikiano pale ujenzi utakapokwama.

Msimamizi wa Mradi toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi Grace Musita amesema ujenzi huo ulitakiwa kukamilika Aprili 2023 lakini umechelewa kutokana na changamoto za ugumu wa ardhi, kupanda kwa gharama za ujenzi.

Amesema “Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2021 kwa gharama ya shilingi bilioni 23.9, tumeshalipwa shilingi bilioni 7.9 tu, ujenzi umefikia asilimia 59.5 na tumefwata taratibu zote za ujenzi kwa kupima vifaa vyote vya ujenzi.”

Waandamana kutaka Rais aondolewe madarakani
Wajawazito 210 wapoteza maisha kanda ya Magharibi